SHARE

Habari yako msomaji  wa blog hii , Ni matumaini yangu kuwa u mzima wa afya na kwamba unaendelea kuongeza bidii katika kujijenga kuwa mtu bora zaidi. Nafurahi na kufarijika  sana kuona kwamba kazi yangu inapokelewa vizuri.

Wiki hii tutaongelea juu ya kujiamini na kujiona mwenye thamani. Katika kipindi cha miaka yako ya ishirini , kujiamini ni muhimu sana na kutachangia katika mafanikio yako. Hivyo nakuletea mambo kadhaa ambayo unaweza kufanya ili uweze kujiamini zaidi.

8fb477be8ea55befdac8a1a712fc70b1

KARIBU

  1. Sisitiza mazuri ya watu na usiwabeze wala kuwatania wale wanyonge na wasio jiamini.  Huwezi kuwa mwenye nguvu wa kuwafanya wengine wanyonge vile vile huwezi kuwa mtu anaejiamini kwa kuwafanya wengine wasijiamini. Kuwa mtu unaewakumbusha wengine thamani yao hasa wale wasioifahamu.

ed6-copy

3.Kumbuka mazuri yako.

Ni rahisi kuona makosa na mapungufu yetu .Kumbuka pia yale ambayo ni mazuri yako. Unaweza usiwe mchezaji bora wa mpira wa miguu lakini ukawa ni mshauri mzuri sana kwa jamaa zako. Tambua hilo na uliboreshe.Kuongeza uwezo wako wa kufanya vitu unavyofanya vema ni muhimu lakini pia usisahau kujifunza kufanya yale ambayo huyajui.

tanzania_jacquelinekibacha_simonmorris_web-jpg-940x528_q85

  1. Shirikiana na familia yako.

Kutoa ushirikiano kwa familia zetu ni muhimu na ni kati ya vitu ambayo kwangu binafsi hunifanya nijiskie vizuri sana. Hivyo ni vizuri kujenga ukaribu na mahusiano mazuri na familia yako.

nakaaya

5.Jisamehe na Omba Msamaha.

Kama binadamu kwa kawaida huwezi kukosa kukosea. Kujuta na kujilaumu visije vikawa tabia yako ya kila siku.  Jifunze Kukubali makosa yako na makosa ya wengine. Chukua mambo haya kama fundisho kwako na usonge mbele.

0fgjhs1t3aa57pve0g-r300x200-7f17f444

6.Tunza afya Yako.

Afya na hali ya mwili ni vitu vinavyofanya vijana wengi hasa wa kike kutokujiamini. Ni muhimu kujikubali vile ulivyo .Lakini ni muhimu pia kutunza afya yako.Kula vizuri, fanya mazoezi, kunywa maji ya kutosha na kupumzika.

wp-1472503325115.jpg

 

7.Jijenge kiroho.

Mambo yote niliyoyataja hapo juu yanahusisha watu wa nje na vitu vya nje.Lakini kujijenga kiroho hukujenga kutoka ndani. Husaidia kujua na kujielewa kwa undani zaidi.

nourishyoursoul1

8.Chagua marafiki zako vizuri

Aliyesema nioneshe rafiki zako nami ntakuambia wewe ni nani hakukosea kabisa. Jifunze jinsi marafiki wanavyoathiri mtazamo wako kwa kubonyeza hapa

CHAGUA MARAFIKI

Na huo ndio mwisho wa post ya wiki hii ,tukutane tena wiki ijayo nikikuletea mada nyingine kwa ajili ya kuboresha miaka yako ya ishirini.

Kama umeipenda post hii usisite ku share na marafiki zako waliopo katika miaka ya ishirini.

Napokea maoni ya kujenga kutoka kwa wasomaji wangu ,ASANTENI SANA.

SAYONARA

LEAVE A REPLY