SHARE

Kati ya mambo ambayo yanafanya tushindwe kuajiriwa ni namna tunavyojiweka tunapoenda katika interview.

Post hii ni muendelezo wa mafunzo kutoka kwa Launchpad Tanzania pamoja na wadau wengine wa soko la ajira na elimu.

Kama hukusoma post za .

Isome hapa kisha tuende sambamba.

MAFUNZO YA UAJIRIKAJI NA UJASIRIAMALI

KUENDA NA KASI YA DUNIA

Ukiachana na mavazi ambayo tunahisi ndo kitu pekee cha kuzingatia unapoenda katika interview , kuna mambo mengine ya kufanya kabla na unapokuwa katika interview.
Kwa kawaida huwa tunatuma CV kwanza kisha tunaitwa katika interview. Kuandaa CV nzuri ni muhimu ili upate nafasi ya kuitwa katika interview. Tuwaletee mfano wa CV nzuri na jinsi ya kuandaa? Share post hii kwa watu wengi uwezavyo na tutaleta somo hilo.

1.Chunguza kampuni ulioomba kazi.

Kīla kampuni ina maono, nia na malengo wanayohitaji kufikia. Pia wana program, mipango na mambo wanayojihusisha nayo. Unahitaji kutumia ujuzi wako katika kufikia malengo haya .Fanya uchunguzi juu ya sehemu yako ya kazi. Uchunguzi huu utakusaidia katika kuweka malengo yako pia. Unaweza ukatuma CV yako cocacola na ukaitwa katika interview ukaulizwa , Cocacola inafanya kazi gani, wewe ukasema inauza soda. Ni kweli cocacola wanatengeneza soda . Hizo soda wanauza wao kama wao ?

Hapana,kuna wasambazaji nchi nzima na wana miradi mingine. Inawezekana wanatafuta mtu wa kuajiri katika miradi lakini wewe unadhani unaenda kuuza soda. Hivyo jitahidi kuchunguza sehemu unayoomba kazi.

2.Jichunguze mwenyewe

Marafiki zako kila siku wanakuambia kuwa upo vizuri katika kupanga na kutimiza mipango mno. Unaingia kwenye interview, unaulizwa kwa nini tukupe hii kazi wewe ?

Unabaki unashangaa.

Fahamu mazuri yako na uwaambie kuwa wewe ni mtu unaweza kufanya kazi katika presha au muda mfupi. Waambie kuwa wewe ni mbunifu na umeweza kutumia ubunifu katika 1, 2, 3.
Usidanganye, chunguza tabia zako nzuri , uzijenge na uzitumie kuajirika.

3.Muda

Kuna namna ya kusoma muda inayoitwa BMT yaani Black man time , Dunia inatumia GMT . Saa mbili ya GMT ni saa nne ivi mpaka saa 6 ya BMT. Unapoitwa katika interview saa mbili na unafika saa tatu tayari unajiweka katika nafasi ya kukosa hiyo kazi.
Kama unafahamu kuna foleni, kwa nini usiwahi kutoka? Uwahi kufika, hata kama umekuja na daladala umekanyangwa una muda wa kujipangusa na kuonekana nadhifu tena. Pia una muda wa kukaa na kutulia na una uwezekano mkubwa wa kutopaniki. Suala la muda ni mada nzima na nusu hasa kwa mazingira yetu. Ni tamaduni mbovu tuliyojenga ambayo inatulemaza na kuturudisha nyuma.

4.ONESHA USHIRIKIANO

Ni kweli hauna ujuzi juu ya Microsoft word, lakini upo tayari kujifunza.
Unapoulizwa unahitaji kulipwa kiasi gani, nategemea uwe umefanya uchunguzi wa mishahara inayotolewa na hiyo kampuni, thamani ya huduma unayotoa na una wastani wa kiasi unachohitaji kulipwa. Hakikisha umechunguza unaweza ukataja kiasi ambacho yule anayemsimamia unamsiamia ndo analipwa hukaishia lkutamani ungejua au mshahara ukawa mkubwa wakashindwa kukuajiri maana hawawezi kukulipa.
Waajiri pia huweza kukupa range ya mshahara na kukuambia uchague , kama range hiyo ipo ndani ya kiwango chako ni vizuri . Inapotokea wanakupa kiasi kidogo zaidi ni uamuzi wako kukubali au kukataa. Unaweza ukaanza na mshahara mdogo lakini mshara wako ukaendelea kupanda unavyoenda.Unaweza kuongea nao juu ya kukuongeza mshahara huo. Unaweza pia ukachukua hiyo kazi wakati unaendelea kutafuta kazi nyingine.

  1. Usirudie kumsomea CV yako

Si ulituma CV , akaona kuwa umesoma Arusha , wewe ni mtoto wa tatu katika familia yenu , una masters ya Medicine na mengineyo. Ndo kakuita , kuna kitu anahitaji kuona zaidi ya kufahamu kuwa ulisoma Arusha ,ukamaliza ukaenda Iringa. Anapokuuliza umuambie kuhusu wewe anahitaji kusikia namna ulivyokuwa unashiriki kati kikundi cha AISEC , ukafanikiwa kufanya kazi na jamii katika mambo kadhaa hivyo una ujuzi wa kufanya kazi na watu, au jinsi ulivyokuwa likizo ulijitolea kwenda kufanya kazi sehemu fulani kwa miezi kadhaa na unafahamu jinsi ya kuendesha shughuli za kiofisi au kwa kazi za ubunifu unaweza ukaonesha mambo ulioyafanya binafsi .
Na hii ni moja kati ya sababu za kujitahidi kutafuta mafunzo ya vitendo pamoja na kupata mafunzo ya darasani. Kujitolea na kujihusisha katika mambo mbali mbali kutakupa ujuzi au experience ambayo inaweza mvutia muajiri.

MENGINE
Piga simu baada ya wiki kuulizia mstakabali wako.
Waeleze ndugu na marafiki kuwa unatafuta kazi, mara nyingine huweza kukutambulisha kwa watu wanaoweza kukuajiri .

Lugha yako ya mwili pia huchangia , unapokaa kaa vizuri na unapozungumza zungumza ukimtazama unaeongea naye.

Sio sasa unamkodolea macho kama unataka kummeza , mtazame ili pia usome kile anachozungumza kwa mwili wake.

Post inayofuata ni kuhusu Ujuzi unaohitaji ili kupata ajira, kutunza ajira au kujiajiri.

Ukiweka email yako hapo inapokuhitaji , utapata taarifa wa kwanza mara tu tutakapopost.

Kama una maswali, maoni au ushauri juu ya mada yetu yaweke katika comments hapo chini.

Tunajitahidi kuleta mada, ujuzi na taarifa kutoka sehemu mbalimbali ili tuweze kukua pamoja, kujifunza pamoja na kuwa watu wazima tuliotaka kuwa tangu utoto. Tunatamani tuwafikie wengi na wewe ndiye chombo na msaada wetu mkubwa. Tusaidie kushea post hii na vijana marafiki .

Tunashukuru

Jifunze zaidi niajiri.co.tz

6 COMMENTS

LEAVE A REPLY