SHARE

Katika post tatu zilizopita , tumefahamu ni kuwa kuna uhitaji wa mabadiliko katika mfumo wa elimu, mtazamo na sera ili tuweze kuendana na kasi ya Dunia na kukabiliana na janga la ukosefu wa ajira.

Kama hujasoma post hizo, zisome kwanza kisha tuende sambamba.

MAFUNZO YA UAJIRIKAJI NA UJASIRIAMALI

KUENDA NA KASI YA DUNIA

NIFANYE NINI NINAPOITWA KWENYE INTERVIEW?

Leo tutazungumzia ujuzi unaohitaji ili kushinda ushindani katika soko la ajira.

Tumezoea kuskia kuwa hatuna ujuzi ama “skills” lakini je tunazifahamu hizo “skills” na tunazitafuta wakati wa mafunzo. Maono ya post hii ni kukupa wewe ujuzi juu ya ujuzi unaohitaji na unaupataje .

Katika mafunzo, Empower pamoja na Niajiri waliongelea umuhimu wa Soft skills katika kupata ajira na kukaa katika ajira. Hizi soft skills ni tabia ya mtu na uwezo wa kufanya kazi na watu wengine.

Hivi ni vitu kama uwezo wako wa kuwasiliana na watu , kutatua matatizo, kufikiri , ushawishi , heshima ya kazi, kusikiliza , kuheshimu ,kubeba majukumu , uvumilivu , kuweza kubadilika na mengineyo.

Mengi kati ya haya unazaliwa nayo au unajifunza siku zinavyoenda pia, kujihusisha zaidi mahali unapokuwepo au kufanya kitu fulani kinachokupa sifa kati ya hizo nilizotaja hapo juu .

Skills nyingine ni zile zinazoendana na ajira yako.

Nitaeleza namna tatu za kupata ujuzi huu.

1. Apprenticeship

Kati ya vitu unavyoweza kufanya unapoenda likizo ni kujifunza kutoka kwa mtu mwenye ujuzi. Jambo hili pia nimeongelea katika kitabu changu. Kujifunza huku hutokea wakati bado upo shuleni au chuo. Unaweza ukalipwa lakini mara nyingi haulipwi .Ni muhimu kujitahidi kujihusisha na hizi program maana ni chanzo kizuri mno cha ujuzi.

Tumeskia watu wengi wakienda kujitolea sehemu kisha wakapata kazi walipomaliza shule au mtu akafanya field mahali na alipomaliza akapata kazi. Ni rahisi kuchukua mtu mliefanya nae kazi kuliko yule anayehitaji kufundishwa.

2. Internship.

Hii ni nafasi ya kupata ujuzi baada ya kumaliza masomo. Kuna masomo yana nafasi hizi na kuna mengine hayana. Ofisi ya waziri mkuu imeweka muongozo wa mafunzo haya ili kuhakikisha kuwa wahitimu wanapata ujuzi wanaohitaji na imeanza na kazi chache za mahotelini.

Lakini kwa sasa, jitahidi uweze kupata aina zote mbili za ujuzi uwezavyo ili uweze kushindana katika soko la ajira .

3.Mentorship

Njia hii hutumia kupata ushauri kutoka kwa watu waliopo katika “field” ya kazi kama yako. Watu hawa wanaweza kuwa walimu au wafanyakazi wengine.

Mentor (anaekufundisha) mzuri anafahamu safari unayoelekea na ana nia ya kukupa ujuzi na ushauri wa kukusaidia kufika mwisho wa safari yako. Ni vizuri uwe na mentor kwa sababu mengi uliyopitia naye alipitia na kuna kitu alichojifunza na yupo tayari kukufunza pia.

Ujuzi ni kama mazoezi , hukujenga zaidi unavyoutumia zaidi. Hivyo jitahidi kutumia ujuzi wako mara kwa mara ili uweze kuunoa zaidi .

Tunaishia hapo kwa leo.

Post ijayo itahusu mada ambayo itafunga mfululizo huu . Mada hiyo ni tofauti na mambo ya ajira za kuajiriwa. Tutazungumza kuhusu kujiajiri na ni Jinsi ya kubuni bidhaa kwa ubunifu.

Tunajitahidi kuleta mada, ujuzi na taarifa kutoka sehemu balimbali ili tuweze kukua pamoja, kujifunza pamoja na kuwa watu wazima tuliotaka kuwa tangu utoto. Tunatamani tuwafikie wengi na wewe ndiye chombo na msaada wetu mkubwa. Tusaidie kushea post hii .

4 COMMENTS

LEAVE A REPLY