SHARE

Dada yangu alikuwa akiniuliza kuhusu marafiki zangu hapo kabla. Kwa umri wangu niliju anafanya kile ambacho dada yeyote angefanya. sasa naelewa zaidi.

Kama ilivyoombwa na mmoja wa wasomaji wa blog hii. Leo tutaongelea mchango wa marafiki katika maendeleo na ukuaji binafsi. Mimi naamini kwamba kukua na kujiendeleza ni kitu muhimu kwa kila mmoja wetu .

Hebu tuangalie mambo haya kuntu kuhusu marafiki.

  1. Marafiki wenye msimamo hukusaidia kujidhibiti                                                                                Marafiki wa aina hii hukupa msukumo wa kufanya vitu ambavyo kwa mara nyingi usingevifanya . Vitu kama kufanya mazoezi , kuomba kuongezewa mshahara  na vingine vingi.                                                                                                                                        Ni muhimu kuwa na marafiki wa aina hii kwani hutunyoosha sana .                  gym.jpg
  2. Watu wenye marafiki wachache hukosa uzoefu wa kijamii wakutosha.  Unapokuwa na marafiki wengi , unaona na kusikia kuhusu maisha katika pande mbali mbali.   4d3cce499144a790106de3bc9a1f1966
  3. Kuwa na mawasiliano mengi katika mitandao ya jamii huongeza msongo. Hii ni tofauti na tulichokieleza hapo juu. Utafiti unaonesha kuwa watu wenye mahusiano mengi katika mitandao ya jamii , huogopa kuwa “offend” watu na hivyo huwa watu wanaotaka kuwapendeza watu wanaowazunguka.RawpixeliStock_796x551.jpg
  4. Kuwa na marafiki wengi huongeza urefu na thamani ya maisha ya mtu  dsc01962
  5. Marafiki wana uwezo wa kubadili mtazamo fikra , imani na tabia zetu .  Inawezekana kuhisi mabadiliko katika mood pale unapoangalia filamu na pengine hata kulia . Hii pia hutokea kwa marafiki. Pale ambapo imani na mtazamo wetu unapopata changamoto , kunakuwa na uwezekano wa kubadilika kwa mitazamo hiyo.
  6. Pia kuna tabia ya kuiga yale ambayo marafiki zetu hufanya . Hii haiishii kwenye matendo tu .Utafiti umeonyesha kuwa tumbili huwa haogopi  nyoka lakini alianza kuwaogopa wakati alipoona  wasiwasi kwa tumbili mwingine.  Hii ina maana kwamba kuangalia mtu mwenye  hisia za hofu, wasiwasi au unyonge inaweza kutufundisha jinsi ya kuwa kama yeye.                              1ae41156b8e6e15815c9a009eedaade1Kama umejizungusha na watu wenye mawazo ya kushindwa , kujifananisha na wengine na kutokuona uwezekano wa vitu basi tunajua mtazamo wako utakapoelekea. Hebu  tujiulize kama marafiki tulionao wanatufanya tuwe watu bora ?  Au swali bora zaidi?Tunawafanya marafiki zetu wawe watu  bora zaidi?                            Asante sana  kwa kusoma blogu hii na kama umeipenda hii posti basi usisite kushare na marafiki zako.                                                                                                                                 Tukutane jumatatu ya wiki ijayo nikikuletea mada nyingine itakayokupeleka katika sehemu bora zaidi uwapo kwenye miaka yako ya ishirini.                                                                                                                                                                                                                                 Sayonara

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY