SHARE

Habari zenu wasomaji was blogu hii. Karibuni katika makala nyingine katika blog hii. Leo tutazungumzia Kansa ya shingo ya kizazi .

Kwa lugha rahisi kabisa ,kansa ni ugonjwa unaosababishwa na kubadilika Kwa seli za sehemu fulani ya mwili. Seli hizi husambaa katika maeneo jirani na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Hivyo Kansa ya shingo ya kizazi (Kwa kiingereza cervical cancer ) ni hali inayotokea katika shingo ya kizazi. Kansa ya shingo ya kizazi ni moja Kati ya magonjwa yanayoongoza kuua wanawake duniani na husababisha ugumba.

Nikiwa shuhuda wa vifo vya wanawake wa karibu , kufahamu kuwa ugonjwa huu una kinga basi ningependa kuwafahamisha kansa ya kizazi ni nini na ni kwa jinsi gani unaweza kujikinga.

Visababishi vya kansa havijulikani bado . Kati ya vitu vinavyochangia ni mfumo wa maisha yani chakuka ,mazoezi nk. Kwa upande wa kansa ya kizazi chakula na mazoezi vina nafasi yake lakini kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengi , kujihusisha na ngono katika umri mdogo (hii huwaweka wasichana wadogo wengi hatarini) huongeza uwezekano wa MTU kuathirika na HPV virus ambae huongeza uwezekano wa MTU kupata kansa ya kizazi .

Turudie tena

Chakula na mazoezi vina nafasi yake lakini kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengi , kujihusisha na ngono katika umri mdogo (hii huwaweka wasichana wadogo wengi hatarini) huongeza uwezekano wa MTU kuathirika na HPV virus ambae huongeza uwezekano wa MTU kupata kansa ya kizazi .Uvutaji wa sigara na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango pia humuweka mtu hatarini.

Baada ya kufahamu hilo niseme kuwa kila msichana na mwanamke ambae anajihusisha na vitendo vya kujamiiana  yupo katika hatari hii.

Dalili za kansa ya kizazi ni pamoja na maumivu wakati wa kujamiiana na kutoka damu, kutoka majimaji yenye harufu mbaya wakati wa hedhi pamoja na siku za kawaida , maumivu katika sehemu za chini za mwili .

Habari njema ni kwamba wizara ya afya inatoa chanjo ya kansa ya shingo ya kizazi bure kwa wasichana kati ya umri wa miaka 9 hadi 13.Hivyo ni vizuri kuwahimiza watoto wetu kupata chanjo hiyo.

Lakini pia kuanzia umri wa miaka 25 unaweza kwenda kupima kwani kansa ya kizazi ikigundulika mapema inaweza kutibika . Wanawake wenye umri kati ya miaka 25 hadi 30 wanahitaji kupima mara moja kwa miaka mitatu na kuanzia hapo wapime mara moja kwa mwaka mpaka watakapofika miaka 50.Baada ya hapo wanaweza kuacha.

Kwa ocean road hospital upimaji huu hufanyika jumatatu mpaka alhamisi kuanzia saa moja mpaka saa saba.

Kupimwa huu kunafanyika bure na tiba pia ni bure kama ilivyo kwa kansa zote. . Ni vizuri ukamuuliza daktari wa magonjwa ya wanawake au fika katika kituo cha afya cha karibu ili upate kipimo hicho.

Nawatakia afya njema na nakaribisha maswali au nyongeza yeyote katika comments hapo chini.

LEAVE A REPLY