SHARE

Baada ya kuandika hii post, nikahisi nimemaliza. Kwamba nimeshawasihi vijana wenye utaalamu fulani kujitahidi kutumia ujuzi huo katika kuboresha mfumo wa kutoa huduma na kuzalisha bidhaa kwa ajili ya wananchi.

Haikuwa hivyo

Dakika chache baada ya kupost hii post, inbox yangu ikafurika na maswali.

Umeniacha njia panda , ina maana unapinga watu ambao wameona vyeti vya chuo haviwapeleki kokote na wameamua kutumia ujuzi wao mwingine kuishi au?

Unafikiri mfumo wetu wa elimu unatufundisha kuona changamoto zinazotuzunguka na kuzitafutia utatuzi ?

Solution yako ni nini? Hayo mabadiliko makubwa yanayohitaji kufanyika ni yapi?

Kila mtu anataka kuishi na kuweza kujikimu yeye na wale wanaomtegemea. Ujue anapotupa cheti chini ya uvungu ni kwamba amekosa namna kabisa.

Hatuna ujuzi na wala hatuutafuti. Semina ngapi za ujasiriamali tumeenda? Somo la Development Studies nalo tumefundishwa ujasiriamali lakini inawezekana tunasubiri serikali itufanyie kitu. Lakini hili halitatokea kwa urahisi wala hivi karibuni. Hivyo cha mihimu ni kufahamu tufanye nini? Nifanye nini ili nisije kupoteza muda kusoma halafu nitupe cheti niuze popcorn ?

Swali likabaki na mimi, Nini sasa? Tufanye nn?

Tanzania ni kati ya nchi yenye vijana wengiiii sana na asilimia mbili tu ya vijana hao hufika elimu ya juu. Kati ya hao wanaofika elimu ya juu, ni wachache zaidi ndiyo huwa na ujuzi unaohitajika na waajiri au wa kujiajiri.Ninayoandika hapa sio mapya, inawezekana wewe ni muhanga wa hili au unaogopa litakapokukuta .

Kukosa ajira ni changamoto kubwa sana kwa vijana wengi , na ni tatizo kubwa zaidi katika nchi za Afrika.

Ni changamoto hii iliwasukuma Carol Ndosi na Henry Kalayu kuanzishathe launch pad tz . Hili ni jukwaa linatolenga kuwasaidia vijana wa kitanzania kupata ujuzi wanaohitaji ili kuajiriwa, tamaduni mzuri ya kazi na uwezo wa kujiajiri pia.

The launch pad tz ilialika wadau mbalimbali wa ajira na ujasiriamali ili kuendesha mazungumzo juu ya ukosefu wa ajira Tanzania.Nia ya mafunzo haya ilikua ni kutoka na orodha ya ujuzi ambao mtu anahitaji ilu kuajiriwa au kujiajiri.Yote haya yanakuja kwa mfululizo katika blog hii.

Wadau hawa ni

  1. Shirika la umoja wa mataifa la misaada kitengo cha kuwezesha vijana kiuchumi

2.Empower : Kampuni ya kuunganisha waajiri na watafuta ajira pamoja na kuwafunza waajiri juu ya ujuzi mbali mbali kuhusu CV kati ya mengine mengi.

3.Shirika la sekta binafsi Tanzania( TPSF)

4.Taasisi ya ujasiriamali na ushindani Tanzania (TECC)

Jukumu kubwa la TECC ni kukuza ujasiriamali, ubunifu, na ushindani nchini kwa kuwezesha maendeleo ya ujuzi na kuunganisha wajasiriamali na sekta za fedha

5.Vijana Think Tank

6.Shirika la kazi duniani

Limekuwa likifanya juhudi mbalimbali za kutengeneza kazi salama na rafiki kwa ajili ya maendeleo stahiki Tanzania.

7.Niajiri

Hii ni kampuni inayofanya kazi ya ku “match” kazi na waajiriwa. Pia hutoa mafunzo ili kumusaidia mtu aweze kuajirika.

8.Sahara Sparks

Hii ni kampuni inayofanya shughuli za kiofisi lakini pia inajihusisha na ubunifu na ujasiriamali wa technolojia .Kati ya program zao ni mawazo challenge . Shindano la ubunifu la wanafunzi wa afya katika kutatua matatizo yanayowazunguka.

9.Ofisi ya waziri mkuu , kazi, vijana , ajira na walemavu ambayo imeweka muongozo juu ya uanagenzi( apprenticeship) na internship. Hizi ni juhudi katika kuhakikisha kuwa wanafunzi hawamalizi mafunzo wakiwa wamejaa kitabu tu bali wawe wamepata mafunzo ya vitendo hivyo kuwa na ujuzi unohitajika.

10.Benki ya Dunia

11.Shirika la waajiri Tanzania ( ATE)

12.Wizara ya elimu

Mijadala yote ilioendelea inakuja katika blog hii . Ikumbukwe pia kwamba Serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu anaehitaji kazi hata kama ana ujuzi hivyo ni jukumu la wadau wa sekta binafsi kutengeneza ajira kwa ajili ya vijana.Kubwa zaidi ni kwamba kuna haja ya mfumo wa elimu kubadilika , mtazamo wa watanzania na hasa vijana wengi kubadilika na kuwepo kwa juhudi za mtu mmoja mmoja kupata ujuzi anaohitaji kwa ajili ya kazi pamoja na kujiajiri hasa tunapoelekea uchumi wa viwanda

Tembelea tovuti za UNAID , Benki ya dunia na Shirika la kazi duniani ili uweze kujifunza zaidi kuhusu matarajio ya kazi , kazi zipi miaka kadhaa ijayo zitakuwa hazihitaji nguvu watu bali mashine, zipi zinazidi kuongezeka uhitaji ? na nini kinafanyika sehemu mbali kukabiliana na mabadiliko ya sasa.

Kumbuka kuweka email yako hapo chini ili upate kutaarifiwa pale tutakapopost.Share post hii pia na marafiki utusaidie kufikia vijana wengi zaidi.

Siku njema

11 COMMENTS

  1. Thanks. I have learned and am following ur posts. May God give u more strength to continue opening minds of many youths in Tanzania about different opportunities available for their development.

LEAVE A REPLY