SHARE

Habari Mpenzi msomaji wa Twentiesco blog,blog pendwa kwa vijana Kati ya miaka 20-29 tukizungumzia mambo mbalimbali kuhusu kujijenga katika vipindi hiki kuelekea Utu uzima.

Mada ya leo ,ni mada kwa ajili ya  kila mtu mtoto kwa mtu mzima hivyo kama ni mara ya Kwanza kufika Twentiesco karibu na kama sio basi Karibu tena na Asante kwa kurudi. Leo tunaongelea  SHINIKIZO LA DAMU maarufu kama “presha”.

Tuanze kwa kuelewa nini maana ya shinikizo la damu.

Shinikizo la juu la damu (HTN) au presha ya juu ya damu (pia huitwa shinikizo la mishipa ya damu , HBP), ni ugonjwa sugu ambapo nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ni kubwa kuliko kawaida. Ongezeko hilo husababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi ili uzungushe damu katika mishipa ya damu . Kwa kawaida halina dalili, ila likidumu lina madhara makubwa kwa afya .(wikipedia)

 

Ni moja Kati ya magonjwa sugu ikiwa na maana kwamba unapopata SHINIKIZO LA DAMU ,huwa hauponi unachoweza kufanya ni kuepuka hali kuwa mbaya zaidi.Na katika kuepuka huku kama ni katika stage za mwanzo,mara nyingi unaweza kuachana na dawa baada ya muda endapo utabadili mfumo wako wa maisha.

Ukiacha presha ya kurithi ambayo kitu pekee unachoweza kufanya ni kuhakikisha hauendei katika hali mbaya zaidi, njia tatu zinazopelekea kupata magonjwa sugu ni chakula , mazoezi na mfumo wa maisha.Kitu kizuri ni kwamba hizi hizi ndio njia za kuepuka magonjwa sugu.

Tuanze na Chakula.

Kuna msemo maarufu kwamba mtu alacho ,ndicho kimjengacho nami siwezi bisha hata thumni

Unapoendekeza vyakula vyenye mafuta ,mafuta hayo hujitunza katika mishipa ya damu na hivyo kuongeza uwezekano wako wa kupata SHINDIKIZO LA DAMU maarufu kama presha. Ni ukweli mchungu kuwa chipsi ,mbuzi choma ,fastfoods nk  ni vyakula vitamu sana tena ni vya kulevya.Kujifunza kuwa na kiasi na kuwa na ratiba ya chakula ni muhimu sana. Jijengee ratiba na uifuate . Kula bila kuruka nyakati za chakula .bila kusahau kunywa maji ya kutosha.

Mazoezi

Huhitaji gym kufanya  mazoezi ,unaweza kukimbia mchaka mchaka katika uwanja wa nyumba unayoishi.Nmekua nikifurahi kuwaona watu hasa Dar es salaam wakiwa wanakimbia mchaka katika pembe za barabara watokapo kazini .Ni njia nzuri kwa mtu busy.kujitahidi kutembea zaidi kuliko kupanda bajaji , bodaboda au lift.Mazoezi unayofanya ni vyema yakaendana na uwezo wako.huwezi anza kwa kukimbia mile 100 lakini ukianza kimbia mile 7 kwa siku 10 .. baada ya miezi minne au sita utakua umejenga uwezo mkubwa.Itakuja post kueleza aina tofauti za mazoezi.

Mfumo wa maisha.

Kila kitu unachokuwa ni zao la yale unayofanya kila siku.Vitu kama unywaji wa pombe na kukasirika haraka hukuweka katika hatari na ya kupata SHINDIKIZO LA DAMU.

Kama huna tatizo la Shinikizo la damu basi ni vyema kuzingatia maeneo hayo matatu muhimu ili kuepuka ugonjwa huu. Nnapoandika hivi nakumbuka maneno yangu mwenyewe kwa rafiki yangu kuhusiana na kula vizuri na kufanya mazoezi.

 Kuwa mnene ni kihatarishi cha magonjwa mengi pia hukufanya uchoke  lakini ishu sio unene ishu ni kuwa na mafuta mengi kuliko kawaida huleta shida  .Mazoezi yatakusaidia uepuke haya magonjwa na hivyo kuongeza urefu na thamani ya maisha. Pia utajiskia mwenye nguvu zaidi.

Mfumo mzuri wa maisha utakuepusha na magonjwa mengi sana.

Ni vigumu kuacha pombe au sigara au mtindo wa kuwaza kupitiliza au kula ovyo ndani ya Siku moja. Lakini inawezekana kwa kuanza Kidogo kidogo.Anza kwa kupunguza kiasi cha pombe unayokunywa au kupunguza chumvi katika chakula Kama una Shinikizo la damu. Badili njia hatari za kujiliwaza na anza njia zenye afya .
Twentiesco ni blog pendwa kwa vijana Kati ya miaka 20-29 tukizungumzia mambo mbalimbali kuhusu kujijenga katika vipindi hiki kuelekea Utu uzima.  Weka email yako hapo chini kabisa ili upate kutumiwa post ya wiki kila jumatatu pamoja na ofa kama vitabu na zaidi.
Tufuate Instagram @twentiescoblog na like Facebook page yetu @Twentiesco.

Je ungependa kuwasiliana nasi moja kwa moja ? Tuma email kwenda twentiescotz@gmail.com

Na hapo tumefikia mwisho wa makala yetu .Nini mtazamo wako katika jambo hili?

1 COMMENT

LEAVE A REPLY