SHARE

 

Siku ya vijana ndio imezinduliwa rasmi leo na Mh. Anthony Mavunde,mbunge wa Dodoma mjini, hapa Dodoma.Ikiwa nimehudhuria kama kijana,mwakilishi wa team ya Twentiesco na UNFPA-YAP , ningependa kuwashirikisha mambo manne ambayo mheshimiwa ameyagusia hususani kwa vijana.

Vijana lazima tujiamini,tuwe na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari,kuzingatia maadili na matumizi mazuri ya muda.

Haya na mengine mengi yameongelewa.

Lakini ,Je wewe kijana mwenzangu,unafahamu hasa nini lengo la maadhimisho haya ya siku ya vijana duniani?ambayo dhima kuu ya mwaka huu 2017 ni  

“Ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika kudumisha amani”

Amani inayogusiwa hapa,si ukosefu wa vita tu! Bali hata amani ndani ya mtu mmoja mmoja…Jiulize wewe una Amani?

Mfano,kijana aliyekosa kazi,au aliye tegemezi baada ya kumaliza shule,hawezi kua na amani na hii huwa chanzo cha ukosefu wa amani hata kwa wanaomzunguka.Naamini mlio wengi hamjawahi kuhudhuria au hata kusikia taarifa zozote kuhusiana na maadhimisho ya siku hii kubwa.Tukiwa siku moja kabla ya maadhimisho hayo, hapo kesho,ningependa kuwaelezea  ni nini hasa lengo la kua na siku hiyo ya kesho. Nikiwekea mkazo majadiliano  yaliyo pendekezwa na vijana kutoka mashirika mbalimbali kama Restless Development, Raleigh,Save the children,Femina ,Global Peace Foundation na nyinginezo nyingi zikishirikiana na wizara ya maendeleo ya vijana.Kuna maeneo makuu sita ambayo ni

1:utawala bora

2: Uwezeshaji kiuchumi

3:  Mchango wa vyombo vya habari katika kudumisha amani

4: Afya ya vijana

5:Elimu na teknolojia

6: Vijana na kudumisha Amani

Haya ni maeneo ambayo yatawaelekeza vijana kutafuta utatuzi wa mambo yanayowakabili huku jamii ikihusishwa.Makubaliano hayo yatapatikana hapo kesho. Ukiwa kama kijana ,mawazo yako ndio ukombozi wako.

Je wewe msomaji unafikiri nini kifanyike ,ukizingatia dhima hii ya “ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika kudumisha Amani?” Ningependa kuona mawazo yako  ili niyawasilishe kwa ajili yakufikia makubaliano ambayo tutayawasilisha  kwa serikali yetu ya Tanzania hapo kesho..

Kijana kua huru kujieleza,Unatakiwa ufahamu wewe ni nani,unaenda wapi na unafika vipi katika malengo yako.

Kuhakikisha kuwa haukosi taarifa zozote katika blog hii , weka email yako hapo chini.

 

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY