SHARE

Katika post nne zilizopita , tumefahamu ni kuwa kuna uhitaji wa mabadiliko katika mfumo wa elimu, mtazamo na sera ili tuweze kuendana na kasi ya Dunia na kukabiliana na janga la ukosefu wa ajira.

Kama hujasoma post hizo, zisome kwanza kisha tuende sambamba.

MAFUNZO YA UAJIRIKAJI NA UJASIRIAMALI

KUENDA NA KASI YA DUNIA

NIFANYE NINI NINAPOITWA KWENYE INTERVIEW?

NAPATA WAPI UJUZI NNAOHITAJI KWA AJILI YA KAZI

Kwangu bidhaa bora ni ile inayosaidia kuboresha maisha, haimfanyi mtumiaji akope na humpa mtengenezaji kile anachohitaji ili aishi.

Sijui bidhaa bora kwako ni ipi? Tueleze katika comments hapo chini.

Katika post zilizopita tumeongelea sana ajira na kuajiriwa . Lakini sasa tutageuza mjadala huu na kuongelea kujiajiri.

Kwa sasa sekta serikali ina uwezo wa kutoa ajira mpya 1000 tu kwa mwaka. Wahitimu wa vyuo wanazidi laki sita kila mwaka na wanazidi kuongezeka. Hivyo tumaini la ajira ni katika sekta binafsi na kujiajiri .

Kama ningekua napewa jero kila muda mtu aliponiambia kujiajiri ni mpango ningekua nimeshanunua kiwanja na kama ningekua ninapewa hata mia mtu aliponieleza jinsi ya kujiajiri , sidhani kama ningeweza hata kununua mshikaki.

Nimesoma somo au topic ya ujasiriamali shuleni mara mbili. Lakini kusoma huku hakuwasha moto wa ujasiriamali kama ilivyokusudiwa. Labda ni kwa sababu mafunzo haya yanahitaji vitu kama kubadili mtazamo ili yaweze kunisaidia na kuwa practical.

Hata hivyo leo, kuna mafunzo kutoka kwa Mwanzilishi wa Sahara Venture , kati ya kampuni zilizoandaa Mawazo Challenge, Jumanne Mtambalike.

Unapohitaji kujiajiri unazingatia nini ?

Mahali ulipo

Kati ya sehemu zenye matatizo katika sekta mbali mbali ni nchi za Afrika. Kuna matatizo ya kisiasa, kiuchumi , kijamii, kiroho na aina zote ambazo unazifahamu wewe. Kuwepo kwa matatizo haya ni nafasi ya ujasiriamali pia. Hivyo kwa kijana wa kitanzania unaweza kuangalia matatizo yanayokuzunguka. Mara nyingi sana watu wapo tayari kukulipa ili uwatatulie matatizo yao.

Ujuzi ulionao

Nitazungumzia pande mbili na utanisamehe kwa kuvutia upande wangu.

Kuna imani kuwa ndoto ni sanaa. Kwamba kama kungekuwa kuna malipo sawa na uhakika sawa katika kazi zote , wote tungekuwa wabunifu, wanamuziki, wachoraji nk. Ili tukishaumwa tufe maana kuwa daktari sio ndoto, au barabara zibaki ni vichochoro maana hakuna mtu mwenye ndoto za kuwa mkandarasi.

Hata hivyo siamini kuwa kazi za sanaa tu ndio zina stahili kuwa ndoto.

Mara nyingi inakua ni tunakosa kwa nini yetu. Tukikosa hii , kuchangia nguvu kazi katika taifa inakua haina maana.

Hivyo ujuzi ulionao sio lazima tuongelee kucheza mpira au kuchora . Ujuzi huu unaweza kuwa ni kutunza rekodi, kutibu, ujenzi, nk. Katika mafunzo huwa tunasoma mambo mengi mno. Hasa kwa elimu yetu hapa Nyumbani. Hivyo tunataarifa ambazo tukiziexploit tunaweza kutoka na suluhisho fulani .

Miezi michache iliyopita wanafunzi wa afya tanzania waliweza kubuni namna za kusaidia kuboresha sekta ya afya . Waliweza kufanya hivyo baada ya kupata mafunzo. Hivyo ujuzi ulionao na ninakazia kwa wasomi kwa sababu tunawategemea unaweza kukupa ajira wewe na vijana wenzako mkiutumia kutatua matatizo ambayo ni mengi mno hapa Nyumbani.

Rasilimali ulizonazo

Sasa tuingie katika kubuni bidhaa. Mambo matatu ya kuzingatia .

  1. Uhitajikaji wa Bidhaa

Je watu wanahitaji bidhaa au huduma yako ? Mara nyingi vitu vinavyowakanyaga watu shingoni na kuwabana huwa wazi .

Foleni barabarani.

Foleni hospitali .

Dhuluma katika ununuzi wa vitu .

Vyote hivi ni nafasi ya kubuni bidhaa au huduma inayotatua shida hii.

Angalia ni namna gani unaweza kutumia Ujuzi wako kutatua matatizo ya watu.

2.Uwezekano

Ningepata bidhaa au machine inayonisomea na kunifanyia mtihani , ni kweli ningeofurahia . Hata hivyo, bidhaa zingine kufanikiwa kwake ni akilini mwetu tu na ni ndoto ( japo kwa sasa)

Hivyo kubuni bidhaa huanza na idea ambayo inaweza ikawa inawezekana au isiwezekane. Lakini katika utekelezaji , uwezekano huchangia mafanikio ya bidhaa.

3.Uendelevu.

Unapobuni , unabuni kwa nia ya kutatua tatizo na kuweza kupata namna ya kuishi . Unapobuni bidhaa isiyoweza kujiendesha na kukutunza wewe hiyo ni hasara. Halikuwa lengo la biashara yako.

Hivyo jitahidi ubunifu wako uingie katika sifa hizo tatu ili iweze kutawala soko .

Ukishakidhi vitu hivyo vitatu tunaanza kupambana na vikwazo kama mtaji , sera nk.

Kitu muhimu pia ni watu walio kwenye timu yako . Unapounda timu , ungana na watu wenye uwezo na ujuzi tufauti unaohitajika katika ubunifu wa bidhaa yenu.

Muda unatengeneza bidhaa hiyo pia ni jambo muhimu. Kunapokuwa na shida ya kitu fulani ndipo biashara hutokea . Kwa mfano, tulikua tukilipa kodi, faini na malipo mbalimbali tangu zamani, hata hivyo tulivyozidi kuongezeka kwa idadi ya watu na biashara malipo yaliongezeka na kulazimisha idea ya Max malipo kukubalika.

Resources

Canvanizer ni website inayokupa msaada katika kutengeneza mpango wako wa biashara.

Kuna sehemu zinaitwa innovation laboratory . Hizi sehemu unaweza kuenda ukakutana na watu wanaokusaidia kutengeneza mpango wa bidhaa yako.

Mfano wake ni Buni Hub ,

Pia kuna siku kunakuwa na maonesho ya ugunduzi mbali mbali, hivyo kuhudhuria au kufuatilia kutaamsha moto wako wa ugunduzi .

Ubunifu au ugunduzi na ufanikishaji wake hutegemea uwezo wa timu yako. Hivyo jiunge na watu wenye uwezo na ujuzi unaongeza thamani katika ugunduzi wenu. Pia kuwa na timu inasaidia katika kushare ile hatari ya biashara.

Ubunifu na Ugunduzi mwema.

Maswali na Maoni juu ya Mada hii yanakaribishwa katika Comments.

LEAVE A REPLY