SHARE

Post hii ni muendelezo wa mafunzo kutoka kwa Launchpad Tanzania pamoja na wadau wengine wa soko la ajira na elimu.

Kama hukusoma post ya kwanza .

Isome hapa kisha tuende sambamba.

MAFUNZO YA UAJIRIKAJI NA UJASIRIAMALI

Miaka 72 iliopita kompyuta ya kwanza iligunduliwa , ikachukua miaka mingine 42 kuweza kutengeneza kompyuta unayoweza kubeba ama laptop. Ikachukua miaka 18 kubuni Macbook air ya kwanza . Lakini ndani ya mwaka mmoja uliopita kumekuwa na mapinduzi makubwa mno ambayo yanazidi kubadili mfumo wa kutoa huduma na bidhaa.

Huu ni mfano katika sekta ya teknologia . Mabadiliko haya tunaweza kuyashuhudia katika sekta za afya, burudani na nyingine. Dunia ya sasa inabadilika kwa kasi mno. Tunaingia katika ngwe mpya ya Zama za mapinduzi ya kidigitali.
Tulianza kabla ya viwanda, tukaingia kwenye zama za viwanda na hatimaye ikaja zama ya digitali .

Kuna utofauti mkubwa sana katika nani anaishi katika zama zipi. Utofauti huu ni mkubwa hasa kwa nchi za dunia ya tatu kama Tanzania japo utofauti huu ni mkubwa zaidi katika nchi kama Afrika Kusini . Na ni muhimu kama mfanyakazi au mfanyabiashara uweke juhudi ya kuwafikia watu katika zama wanayoishi ili tutimize malengo ya maendeleo endelevu. Hata hivyo kwa sababu ya mabadiliko ya mfumo wa kupata taarifa , hufungwi na mji wala nchi.

Tumekuwa sio tena wananchi wa nchi zetu bali wa mabara yetu na Dunia. Na mambo yanayotokea sehemu nyingine yanatuhusu kwa kiasi kikubwa.

Hii ni moja ya sababu za kukufanya wewe ufuatilie kwa ukaribu ili kuendana na kasi ya Dunia. Bila kufanya hivyo Dunia itakuacha. Na kama muajiri,mfanyabiashara, mjasiriamali, muajiriwa na binadamu tu wa kawaida ni muhimu kuenda au kufahamu muelekeo wa sayari unayoishi juu yake.
Unawezaje kufanya haya?

1.KUBALI

Kubali kasi ya mabadiliko na uendane nayo ukiwa na nia,kasi na madhumuni yako . Ni kweli ilikuwa lazima kutuma pesa kwa basi miaka kadhaa iliyopita lakini je Leo hii kuna ulazima huo ?
Kuna mambo mengi ambayo bado yanaendelea kutokea ingawwa kuna chaguo nzuri zaidi ila tu ni sababu tumeamua kukaza vichwa na kufunga akili.

2. NENDA KUSIKOJULIKANA

Umewahi kuogopa kufanya kitu kwa sababu ni kipya ? Au sababu huna uhakika kitaendaje?

Ni muhimu kuachana uoga huu na kuingia pale usipokuwa na uhakika. Sisemi kuwa ni lazima uanze kutafuta vitu 200 usivyovijua na kuvifanya, hapana ila kuna vitu unavyokutana navyo kama vile nafasi za kujifunza kitu kipya, kukutana na watu wapya na kuwa katika timu flani au kikund fulani. Vingine ni vile unavyotaka mwenyewe kama kufahamu kitu fulani au kuanzisha biashara au kitu kipya. Unapoingia usipokujua unajifunza mambo mengi mapya, unakua jasiri zaidi , kukutanisha na watu wapya na vinakujenga kwa ajili ya baadae.

3.KUWA NA NJAA YA MAARIFA NA UISHIBISHE

Kati ya nyakati ambazo zina urahisi wa kupata taarifa na maarifa ni sasa. Unaweza kujifunza mambo mengi sana katika simu yako.Ni chaguo lako unapata maarifa gani , muda gani na kwa kiasi gani. Unaweza ukajifunza kidogo au ukawa mtaalamu kabisa. Kila siku namna ya kufanya vitu inaboreshwa hivyo ni muhimu kuendana na mabadiliko na maboresho hayo

4.POKEA MAMBO MAGUMU NA UKUE KUTOKANA NAYO.

Kwa sababu Yapo.

Kila unapokutana na vitu vigumu unaweza kuvutiwa kurudi nyuma na kuacha. Lakini ni vyema zaidi ukavipokea iwe ni kushindwa, mabadiliko ya sheria na taratibu zinazoathiri kazi au biashara yako n.k . Carol Ndosi ameongelea jambo hili hapa.

BARUA KWAKO MJASIRIAMALI UNAYEANZA

Post ijayo itakayohusu Tamaduni nzuri ya Kazi na namna ya kujiweka unapoenda katika Interview.

Ukiweka email yako hapo inapokuhitaji , utapata taarifa wa kwanza mara tu tutakapopost.

Kama una maswali, maoni au ushauri juu ya mada yetu yaweke katika comments hapo chini.

Tunajitahidi kuleta mada, ujuzi na taarifa kutoka sehemu mbalimbali ili tuweze kukua pamoja, kujifunza pamoja na kuwa watu wazima tuliotaka kuwa tangu utoto. Tunatamani tuwafikie wengi na wewe ndiye chombo na msaada wetu mkubwa. Tusaidie kushea post hii na vijana marafiki .

Tunashukuru .

8 COMMENTS

  1. “I can not afford to fail ,and if I do ..I will not fail again”.
    I love this spirit of Carol Ndosi…I wish all of us could have this kind of winning spirit.
    Nice post …

  2. Always let us return by rising others, their charisma, integrity, and compassion will rise us too. Our hands shakes each other and our gratitude keeps us on track. I will rise from you who rises me up. Thanks good motivational messages

LEAVE A REPLY