SHARE

 

NINI MAANA YA KUPAMBANA NA HALI YAKO BILA KUTINGISHA YANGU?
Kama kuna kamsemo nimekaskia sana hivi karibuni ni pambana na hali yako . Ukakaa af ukaongezewa na kuwa pambana na hali yako bila kutingisha yangu.
Leo tutachambua ni jinsi gani unaweza kupambana na hali yako bila kutingisha yangu.

Kwanza kabisa Karibu katika blog ya Twentiesco .Mambo yote kuhusu safari ujana , tukizungumzia hapa. Lengo ni kuweza kufikia pale ambapo tunataka kuwa. Hakikisha unaeka email yako hapo chini ili ujulishwe pale kunapokua na post mpya na vingine vingi.

Kupambana na hali ni kupigana ili kuepuka,kuachana na au kutafuta suluhu kwa changamoto fulani. Changamoto hizi huja katika njia tofauti kama vile maisha,masomo,kazi,mahusiano kati yetu na watu wengine ,Mungu na hata sisi binafsi.

Kutafuta nafuu ni asili ya binadamu hivyo kupambana ni lazima kutokee.

Na namna ya kupambana hutofautiana kati ya mtu na mtu .Mazingira nayo yana mchango wake katika maamuzi . Hili ni somo la siku nyingine.

Mambo makuu matatu ya kufanya ili usitingishe hali ya mwenzako ni

1.Tambua kuwa kila mtu ana hali yake.

Tena nyingine kubwa tu.

Hata kama hajakuambia ana hali

Unamuona yupo yupo tu ,ana hali yake

Amefurahi kila siku ,ana hali yake

Amekaa kama amekamilisha kila kitu naye ana hali yake huyo.
2.Heshimu kupambana kwao
Tumepitia na tutaendelea kupitia ugumu fulani wakati Fulani.Kutokua na hali fulani sio sababu ya kumtizama mwingine na kumuona ni wa ajabu .Heshimu juhudi zao katika kupambana huko.Kama huongezi chochote ni bora ukakaa kimya.

3.Pambana na hali yako bila kutingisha ya mwingine.

“Misery loves company”

Inawezekana ukaanguka, ni rahisi kabisa kutamani kuwavuta wengine. Kataa kufanya hivi , Msaada utatoka wapi sasa kama wote mpo chini. Wala kutafuta mwenye hali mbaya zaidi ili ujiskie vizuri.Kwani hali yako imebadilika?
Maoni yako ni nini? Unapambana vipi na hali yako bila kutingisha ya mwingine?

Acha comment apo chini. Bila kusahau kushea hii link na kuweka email yako hapo chini.
Wiki Njema

5 COMMENTS

 1. Post ya leo nimeielewa, Kumbe wanavyosema upambane na hali yako si wanakuwa wanakutenga ila wanakufanya uvumbue mbinu nyingi za kujitoa pale ulipokuwa upo..
  “To become ‘unique,’ the challenge is to
  fight the hardest battle which anyone can
  imagine until you reach your
  destination.” A. P. J. Abdul Kalam

 2. Kwa kifupi, huu msemo nimeupenda sana, kwani umekua ni chachu ya watu kupambana na changamoto za maisha zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku. Ukitumiwa positive basi ni msemo unaoenda kuwainua wengi kutoka katika hali zao duni na kufikia malengo yao ya sasa na hata ya baadae.

 3. Hii post imenivutia saana. Nimeona watu wengi wakiona wameshindwa na kulemewa na hali zao wanaanza kutingisha hali za wengine ili waanguke kama wao. This thing is not good for sure. Vijana embu tupambane na hali zetu jamani.

LEAVE A REPLY