SHARE

Habari zako msomaji wa blog hii, Napenda kukushukuru kwa kusoma blog ya Twentiesco . Natumaini unayoyasoma hapa yatakusaidia katika miaka yako ya ishirini. Kama utapenda post hii basi usisite kuwatonya wenzako ili nao wasikose mambo haya kuntu .

Posti hii ni muendelezo wa posti ya hatua kuu nne za maisha tuliyoisoma wiki jana. Kama hukuisoma basi Bonyeza hapa ili kuioma kusudi tuende pamoja. KARIBU
Inabidi ieleweke kuwa stage za mwanzo hazichukui nafasi ya stage za zilizopita..Waliopo katika hatua ya pili sio kwamba hawajali jamii inawachukuliaje wanajali kitu zaidi ya mtazamamo wa jamii . Wao hujali kuvuka limits na kufanya vitu vikubwa.

JELA ILIVYOMBADILI LULU

Waliopo hatua ya tatu pia wanajali kitu kikubwa zaidi ya kufanya mambo makubwa , wao hujali commitments zao .

Waliopo hatua ya nne vile vile wao huwa na utimilifu zaidi wakijali ni vipi watafanya yale walioyaishi yaendelee kuishi.

Unapohama kutoka hatua moja kwenda nyingine , mahusiano yako na vitu unavyojali pia hubadilika. Na ndio kitu kinachosababisha kupoteza marafiki na  kubadili mahusiano. Ni muhimu kufahamu hili ili usilazimishe vitu .

HATUA NNE ZA MAISHA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

Kama wewe pamoja na rafiki zako mlikuwa katika hatua ya kwanza ,kisha wewe ukatulia na ukapata commitments basi bila shaka Kutakua na utofauti wa mambo mnayoyapa kipaumbele utakaofelisha mahusiano yenu.

Kuhama kutoka hatua moja hadi nyingine husababishwa na trauma ,tukio hasi ,kukaribia kupoteza maisha ,kuvunjika kwa urafiki au  kupoteza mpendwa.

HATUA NNE ZA MAISHA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

Mambo  haya humfanya mtu aangalie ni vipi anatafuta furaha. Na kama njia hiyo inamletea furaha. Pia mtu huangalia msukumo na maamuzi yake na kuyafanyia kazi .
Kila mtu huakisi hatua aliopo kwa wengine. Mtu aliye hatua ya kwanza hujaji watu kutokana kiwango chao cha kukubalika katika jamii.

Vile vile watu waliopo hatua ya pili hujaji watu kutokana na uwezo wao wa kufanya mambo makubwa na kuvuka vikomo vyao.

HATUA NNE ZA MAISHA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

Walio katika hatua ya tatu hujaji watu kutokana na commitments walizojiwekea.

Na wale waliopo hatua ya nne hujaji watu kutokana na yale wanayoamini na walioamua kuyasimamia.

HATUA NNE ZA MAISHA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

Ni nini hukwamisha watu katika hatua hizi?

Kutohisi kuwa wanatosha na wamefanya vya kutosha.

Watu waliokwama katika hatua ya kwanza huona kuwa bado wana uhitaji wa kukubalika na jamii. Hivyo hubaki wakijaribu kumfurahisha kila mtu na kufuata viwango na mategemeo ya jamii bila kuona kwamba imetosha. Haitokaa Itoshe.

Waliokwama katika hatua ya pili huona kuwa hawajajipima vya kutosha wala kufanya mambo makubwa vya kutosha. Wao huendelea kufanya vitu vinavyopima uwezo wao. Bila kuona kuwa inatosha.

Wanaokwama katika hatua ya tatu huona kwamba hawajafanya vyema katika maeneo waliyochagua . Hujitahidi kadri ya uwezo wao lakini bado huona haijatosha.

Na hatimaye wanaokwama katika hatua ya nne ,tunaweza kusema kuwa huogopa kwamba Urithi waliouacha hautoshi . Hutumia kila pumzi yao wakiweka msisitizo kwa yale waliyoyasimamia. Pamoja na kufanya hivyo kamwe hawaoni kuwa imetosha.
Tufanye nini sasa?

Jawabu la swali hili linapatikana kwa kurudi nyuma.


Ili kutoka hatua ya kwanza inabidi ukubali kwamba hauwezi kuwa wa kutosha kwa kila mtu masaa yote.Inabidi ujifunze kuamua bila kujali viwango na mategemeo ya jamii.

Ili kutoka hatua ya pili ,inabidi ukubali kwamba huwezi kutimiza kila ndoto na tamaa yako. Hivyo uchague vile vya muhimu na kujicommit kwa hayo.

HATUA NNE ZA MAISHA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

Ili kutoka hatua ya tatu ,inabidi ufahamu kuwa muda na nguvu yako zina kikomo. Hivyo ni vizuri ukatumia mda huu kufundisha kazi na project zako kwa watu wadogo .

LULU ANA FURAHA

Na kusudi uweze kutoka hatua ya nne , inabidi ukubali kuwa nguvu ,ushawishi na msimamo wa mtu hata awe mkubwa vipi. Mwisho hupotea tu.

Na Maisha yataendelea.

Tukutane wiki ijayo nikikuletea mada nyingine. Kama ungependa kuuliza swali au niandike post kuhusu kitu fulani basi niambie katika comments hapo 👇🐈

SAYONARA

LEAVE A REPLY