SHARE

Habari yako ,Ni matumaini yangu kuwa u mzima wa afya. Wiki hii nakuletea hatua nne kuu katika maisha ya Binadamu . Karibu na asante kwa kusoma blog hii.

  1. UIGAJI

Katika hatua hii ya kwanza sisi ni wanyonge, hatuwezi kuzungumza, kutembea au kujilisha wenyewe. Sisi hukopi kutoka kwa wazazi wetu au walezi wetu. Watu wazima katika jamii inayotuzunguka hutusaidia  kufanya maamuzi na kuchukua hatua wenyewe.

Lakini baadhi ya watu wazima na wanajamii inayotuzunguka hutuadhibu kwa uhuru wetu. Hawana msaada katika  maamuzi yetu. Na kwa hiyo hatuwezi kuendeleza uhuru huo. Hivyo tunabaki tukiwaiga wale walio karibu nasi, bila kukoma kujaribu kuwaridhisha  wote ili tukubalike

Sisi pia hujifunza kuishi katika jamii  tukifanya  shughuli zetu za kila siku. Uigaji huu unaendelea mpaka ujana au mwanzo wa utu uzima . Kwa baadhi ya watu, inaweza kuendelea hadi anapokuwa mtu mzima. Wachache huamka siku moja wakiwa na miaka 45 na  kutambua kuwa hawakuwahi kuishi kwa ajili yao wenyewe huku wakishangaa miaka imeenda wapi.

LIFE STAGES AND WHAT TO DO ABOUT THEM

Katika hatua hii  kuna kutafuta  uthibitisho. Hamna misingi binafsi wala uhuru. Katika hatua hii tunajifunza  viwango vya jamii na matarajio lakini ni lazima pia kujifunza kutenda licha ya viwango na matarajio hayo. Ni lazima pia kujenga  uwezo wa kutenda na kufikiri  wenyewe.

  1. Kujitambua

Katika hatua hii sisi hujifunza utofauti wetu. Tunaanza kufanya maamuzi na kujipima wenyewe. Hii inahusisha makossa, kesi na majaribio, kishi katika maeneo mapya na kukutana na watu wapya.

Baadhi ya mambo haya huenda vizuri na mengine vibaya. Ni vizuri kushikilia yale mazuri na kusonga mbele. Hatua hii huendelea mpaka tunapokutana na kikomo. Ni vizuri hatua hii ikianza mapema .

spring-summer-font-b-military-b-font-style-font-b-pink-b-font-camouflage-t-shirt

Tunapokaribia mwisho  wa hatua hii, tunagundua mambo ambayo ni mabaya  na ambayo ni mazuri kwa muda. Mambo kama ngono, kusafiri na kunywa. Hii hatua huendelea mpaka miaka ya thelathini.

KUMBUKA

Baadhi ya watu ni hukwama katika hatua hii

Kufikia kikomo ni muhimu kwa sababu ni lazima hatimaye  kutambua kwamba wakati wako katika dunia hii ni mdogo na unapaswa kututumia kwenye mambo muhimu zaidi. Ni muhimu kutambua kwamba kama unaweza kufanya kitu, haina maana unapaswa kufanya hivyo. Kutambua kwamba kwa sababu tu wewe ni kama watu fulani haina maana unapaswa kuwa pamoja nao. Pia kutambua pia kwamba kuna gharama kwa kila kitu hivyo huwezi kuwa na yote.

Kuna baadhi ya watu ambao kamwe hawajiruhusu kufikia kikomo- ama kwa sababu wanakataa kukubali makosa yao, au kwa sababu ya kujiaminisha kwamba hawana kikomo .Watu hukwama katika hatua ya pili.

Hawa ni wale ambao wana miaka  38 na wanaishi na wazazi wao bila kuingiza  fedha yoyote baada ya miaka 15 ya kujaribu. Hawa ni watu ambao hawawezi kukaa katika uhusiano wa muda mrefu kwa sababu daima kuna mtu bora Zaidi.

Mimi nipo katika hatua ya pili.  Napenda kujua katika comments  jinsi hatua hii inavyoenda  au ilivyoenda kwako .

  1. kujitoa

Watu wengi kuacha burudani ,marafiki na shughuli zisizo na maana.  Kile unachokiacha nyuma,  ndicho watu watakumbuka nacho. Utaiacha vipi dunia tofauti na ulivyoikuta?

 

Kwa kawaida hatua ya tatu ujumla hudumu kutoka miaka ya thelathini mpaka mtu anapofikia umri wa kustaafu.

Watu ambao hubaki katika hatua hii hutaka Zaidi na Zaidi. Hutamani kuzuia asili au kusimamisha muda na huendelea mpaka miaka ya sabini na themanini.

  1. Urithi

Hatua hii inahusisha kufanya  yale ambayo umeshayafanya kupitia kushauri na kufundisha miradi yako  kwa wale walio chini yako.

Una uwezo mkubwa wa kujitawala katika hatua hii.

a22b67db9c414ad3083a7f69723de8a2

Hatua Nne ni muhimu kisaikolojia kwa sababu kama binadamu, tuna haja ya kuhisi  kwamba maisha yetu yalikuwa na maana.

KUMBUKA

Hatua hizi hutokea tofauti kwa kila mtu . Pia kuna mabadiliko ambayo hutokea unapohama kutoka hatua moja kwenda nyingine.

UNAFIKIRI UPO KATIKA HATUA GANI? Ningependa kujua.Tupia maoni yako hapo kwa comments.

Asante kwa kusoma blog yangu. Kama umeipenda post hii usisahau kufollow hii blog kupitia e-mail yako . Share post hii na marafiki zako pia.

Tukutane katika post ya wiki inayofuata.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY